Monday, April 16, 2012

Vijana watakiwa kujenga utamaduniwa wa kujitolea shughuli za maendeleo

VIJANA wametakiwa kujenga utamaduni wa kujitolea na kutoa michango katika shughuli mbalimbali za kijamii bila kusubiri kusukumwa kufanya hivyo.

Wito huo umetolewa na Meneja Masoko wa Chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM), Dk Omary Mbura alipokuwa akitoa mada katika warsha iliyowahusisha wanafunzi wa chuo hicho jana jijini.
Alisema , vijana hawana budi kutumia nguvu , jitihada na uwezo wao katika kuchangia shughuli za kijamii ili taifa linufaike kupitia wao kwa kuwa sehemu kubwa ya maendeleo ya nchi inategemea nguvu kazi ya vijana.

“Vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa ni jukumu la kila mmoja wenu kwa nafasi yake kuhakikisha anachangia katika shughuli za kijamii, lengo ikiwa ni kuliletea maendeleo taifa ambalo kwa kiasi kikubwa linategemea utendaji kazi mzuri wa vijana”alisema Mbura

Aliongeza kuwa , sehemu kubwa ya vijana wanaomaliza katika chuo hicho wanaenda kuwa viongozi katika sekta mbalimbali hivyo hawana budi kutumia mafunzo waliyopata kuwa mfano bora katika kulilietea taifa maendeleo.

Naye Muhsin Masoud ambaye alikuwa mwezeshaji katika warsha hiyo alisema, wakati umefika sasa kwa vijana kubadilika na kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yatakuwa na mchango mkubwa kwa taifa.
Alisema vijana hawana budi kupingana na mmomnyoko wa maadili ambao unaonekana kushika hatamu kwa sasa na badala yake wazingatie maadili pamoja na kanuni ambazo hazina lengo la kupindisha sheria.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment