Friday, June 27, 2014

WAKULIMA WAFUNDISHWA JINSI YA KUANDAA UDONGO WA KITALU

Shirika la FASO likishirikiana na mtaalamu wa kilimo kutoka shirika la TAHA wametoa elimu kwa wakulima wa kijiji cha Ngasinyi, Moshi vijijini. Katika elimu hiyo Afisa kilimo kutoka shirika la TAHA, ndugu Gilliard alitoa elimu ya kuandaa udongo kwa kuuchoma udongo ili kupunguza wadudu.  Elimu hiyo itawawezesha wakulima kutotumia dawa za kemikali katika kukabiliana na wadudu. Hatua hiyo ni mwanzo wa shamba darasa la nyanya litakalo andaliwa kwapamoja.

Wakulima wakiandaa udongo kwa ajili ya kitalu.


Udongo ukichemshwa ili kuua wadudu.

Wakulima wakishuhudia udongo unavyochomwa

Afisa kilimo kutoka TAHA, Ndg Gilliard akikoroga udongo


Udongo ukipakuliwa teyari kwa kuanza kutumika

Afisa kilimo akiupooza udongo uliochomwa.

Thursday, June 26, 2014

WAKULIMA WAPATIWA MAFUNZO YA KILIMO HAI


Wakulima wa kata ya Kahe, Moshi vijijini wapatiwa mafunzo ya kilimo hai chini ya mradi unaofadhiliwa na shirika la Thefoundation for Civil Society na ILO na kutekelezwa na shirika la FASO lenye makazi yake Moshi, Kilimanjaro-Tanzania.  Mafunzo hayo yalitolewa na mwezeshaji kutoka shirika la FROLESTA Bi. Fatuma. 



Bi. Fatuma, mwezeshaji kutoka shirika la FROLESTA akifundisha somo la kilimo hai kwa wakulima wa Kahe



Ndugu. Calvin Salema kutoka FASO akizungumza na wakulima wakati wa semina ya Kilimo hai.



Shamba darasa la kutengeneza mbolea ya mboji