Shirika la FASO likishirikiana na mtaalamu wa kilimo kutoka shirika la TAHA wametoa elimu kwa wakulima wa kijiji cha Ngasinyi, Moshi vijijini. Katika elimu hiyo Afisa kilimo kutoka shirika la TAHA, ndugu Gilliard alitoa elimu ya kuandaa udongo kwa kuuchoma udongo ili kupunguza wadudu. Elimu hiyo itawawezesha wakulima kutotumia dawa za kemikali katika kukabiliana na wadudu. Hatua hiyo ni mwanzo wa shamba darasa la nyanya litakalo andaliwa kwapamoja.
Wakulima wakiandaa udongo kwa ajili ya kitalu.
Udongo ukichemshwa ili kuua wadudu.
Wakulima wakishuhudia udongo unavyochomwa
Afisa kilimo kutoka TAHA, Ndg Gilliard akikoroga udongo
Udongo ukipakuliwa teyari kwa kuanza kutumika
Afisa kilimo akiupooza udongo uliochomwa.
No comments:
Post a Comment