Monday, September 13, 2010

UFAFANUZI

“KILIMO KWA CHAKULA AJIRA NA MAENDELEO,KWA PAMOJA TUNAWEAZA"


Jina la kikundi: FUMBUKA Agro Solution Group.

Jina la Ufupisho: FASO Group

Jina la mwanzilishi: Innocent John Mbele.

Makao Makuu ya kikundi -kata ya KAHE, kijiji cha Ngasini.

Eneo la shughuli za kikundi -Moshi Vijijini.



Utangulizi;

FASO ni kikundi kilichoanzishwa kwa lengo la kuwaunganisha wakulima wadogo (hususani vijana) ili waweze kujihusisha na kilimo cha uwakika kwa pamoja. Kikundi hichi kilianzishwa na ndugu Innocent J Mbele akishilikiana na vijana wenzake ambao ni Fredrick Mahinya. Mchakato wa kuanzisha kikundi hichi ulianza mwezi februari,2010.Kikundi kilisajiliwa rasmi 30/04/2010 na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya moshi vijijini na kupewa na


NIA NA MADHUMNI YA KIKUNDI.

a) Kuunga mkono mapinduzi ya kilimo kupitia sera ya Serikari ya “kilimo kwanza”, kwa kuwahamasisha vijana wajihusishe na shughuli za kilimo.

b) Kuwaunganisha vijana katika vikundi vidogo ili waweze kujihusisha na kilimo cha pamoja.

c) Kukodisha pembejeo za kilimo na mashamba kwa wanakikundi kwa masharti nafuu.

d) Kutafuta Soko la uwakika la mazao yanayolimwa na wanakikundi na jamii ya wakulima inayowazunguka.

e) Kuhimiza kilimo cha uwakika kisicho tegemea mvua (kilimo cha umwagiliaji)

f) Kuwaunganisha wanakikundi na wataalamu mbalimbali wa kilimo ili kupata elimu ya kilimo cha kisasa pamoja na elimu ya ujasilia mali.

g) Kuhifadhi na kusindika mazao yalimwayo na wakulima.

h) Kutoa mchango wa maendeleo ya jamii mfano kuchangia chakula mashuleni upandaji wa miti pembezoni mwa vyanzo vya maji, utoaji wa elimu ya Ukimwi kwa jamii husika n.k .


Mikakati

“Kuongeza upatikanaji wa chakula, ajira na Maendeleo kwa vijana na jamii inayowazunguka kwa ujumla”

Mipango

“Kuondoa umaskini kwa kuboresha kilimo kupitia usambazaji wa pembejeo na utoaji wa taarifa za kilimo pamoja na masoko kwa wakulima wadogo”

Dira

Maono ya kikundi ni “kuwa taasisi/ shirika lisilo la kiserikali ambalo litashawishi Maendeleo ya kilimo Tanzania kwa kutoa taarifa mbalimbali za kilimo, kusambaza pembejeo na kutoa huduma za kijamii kwa wakulima ”

Kauli mbiu

“Kilimo kwa chakula, ajira na Maendeleo kwa pamoja tunaweza”

SIFA ZA MWANAKIKUNDI

-Awe kijana mwenye umri kati ya miaka18-35

-Awe mwenyeji wa eneo la mradi.

-Awe mwaminifu/asiwe mwizi na mwongo.

-Awe na akili timamu.

-Awe anapenda ushirikiano.

-Awe mchapakazi.

-Asiwe mlevi kupita kiasi.

-Awe mtanzania.

-Asiwe mbaguzi wa rangi, kabila, ukoo au jinsia.

-Atambulike na uongozi wa mtaa /kijiji/ kata.

Majukumu (wajibu) wa Mwanakikundi

-Kushirikiana na wenzake kufanya kazi za kikundi

-Kulinda mali za kikundi .

-Kutoa michango mbalimbali itakayotolewa na kikundi.

-Kushiriki katika kazi za kijamii.

-Kubeba dhamana ikiwa janga lolote litatokea.

-Kulipa gharama za upotevu wa makusudi wa mali za kikundi

Haki za Wanakikundi

i) Kushiriki katika shughuli zote za kikundi hiki kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

ii) Kutoa maoni yake katika mikutano ya kikundi hiki.

iii) Kuchaguliwa kuwa mjumbe /kiongozi na kuchagua wajumbe /viongozi wa chama hiki.

iv) Kupitia masharti, mizania, muktasari ya mkutano mkuu na nyaraka zote na taarifa za mwezi na mwaka za kifedha.

v) Kununua hisa za kikundi kwa idadi isiyozidi (2/5) 40% ya hisa zote za kikundi.

7.4 Kusimamishwa au kuachishwa Uanakikundi.

-Kushindwa kushiriki katika kazi za kikundi bila taarifa / sababu yeyote.

-Kufanya kitendo chochote ambacho bodi itaridhia kuwa ni cha kutokuwa mwaminifu ambacho ni kinyume na madhumuni ya uanachama

-Kushindwa kufikia kiwango cha hisa kilichoweka kwa mwaka.

-Kukisababishia kikundi hasara kwa uzembe wa makusudi.

-Kutoudhuria mkutano mkuu wa kikundi mara tatu mfululizo bila sababu ya msingi.

7.5 Uwanakikundi Utakoma kwa :-

a) Kujiuzulu mwenyewe baada ya kutoa taarifa kwa maandishi kwa bodi ya Uongozi.

b) Kifo.

c) Kuchukua hisa zake zote kikundini.

d) Wazimu uliothibitishwa.

e) Akiama eneo husika.

f) Kukataliwa uanachama na theruthi mbili (2/3) ya wanachama walioudhuria mkutano mkuu baada ya kupewa nafasi ya kujitetea baada ya kutenda makosa ambayo yanalazimu kukataliwa uwanakikundi

g) Kufilisika kwa Kikundi.

h) Mtu aliyeacha au kufukuzwa uwanakikundi anaweza kujiunga tena kwa mujibu wa masharti haya. Hata hivyo mwanakikundi aliyewahi kujiuzulu/kufukuzwa itabidi apate idhini ya mkutano mkuu ya kujiunga tena na kikundi.

Vikundi Vidogo Vidogo

- Vitakuwa na wanakikundi 3.-6.

-Kila kikundi kitaandaa mchangano wa kilimo/ufugaji wanaotaka kuufanya na gharama zake.

-Kikundi kitashirikiana na kufikisha taarifa za utendaji mara kwa mara kwa katibu wa kikundi.

-Kila kikundi kitapanga eneo la uendeshaji wa kilimo/ufugaji na kukaguliwa na kupitishwa/ kukataliwa na bodi ya uongozi.

-Kila kikundi lazima kiwe na msichana angalau mmoja au zaidi

-Kila kikundi kitamchagua msimamizi /mwakilishi wake mmoja.

FEDHA ZA KIKUNDI.

-Fedha za kikundi zitatokana na

. A) Kiingilio,ada na michango maalumu. B) Ruzuku na misaada C) Hisa za wanakikundi D) Ziada halisi. E) Mikopo kutoka mabenki na taasisi nyingine

-Kiingilio katika kikundi ni Tshs 1000/= kwa kila kikundi.

-Ada ya uwanakikundi ni Tshs 3000/= kwa mwaka.

-Kila mwanakikundi anaruhusiwa kuwa na hisa katika kikundi.Kila hisa moja ina thamani ya Tsh 3000/=

-Kila msimu kikundi kitatenga asilimia 12% kutokana na faida halisi kwa ajili ya mfuko wa ukuzaji wa mtaji.

-2% kutoka katika faida halisi kwa ajili ya mfuko maendeleo ya jamii (Social development fund)

-2% katika faida halisi kwa ajili ya mfuko wa bima ya kikundi.

-1% ya faida halisi ya kikundi/vikundi vidogo vidogo kwa ajili ya mfuko wa Elimu ya kilimo.

Anwani

Kahe-Moshi, Tanzania

Simu: 0715 571 301 or

0765 571 301

Barua Pepe: faso.group@yahoo.com

No comments:

Post a Comment