Kuajiriwa
na kujiajiri ni changamoto kubwa zinazomkabili kijana ambaye yuko
shuleni/chuoni na anatarajia kumaliza masomo yake baada ya muda
mfupi. Vijana wengi wamekuwa wakifikiri waajiriwe wapi na kwa
mshahara kiasi gani, katika biashara gani ambayo itawaingizia kipato
cha kujikimu.
Kilimo
ni moja ya shughuli rasmi ambayo kijana anaweza kujiajiri na kupata
kipato. Ila ni vijana wachache ambao wamewahi kufikiri kuwa kilimo
kinaweza kuwakomboa katika umaskini wa kipato. Kilimo kimedhaniwa
kuwa ni shughuli inayofanywa na watu wanaoishi vijijini ambao
hawajasoma na wamekosa uwelekeo katika maisha. Ndio maana mtu
akiyumba katika maisha awapo mjini au akifeli shule watu humshauri
aende kijijini akalime. Shughuli za kilimo zimechukuliwa kuwa ni
shughuli ambayo haihitaji utaalamu. Mashuleni, mitaani na Vyouni,
vijana wengi wamekuwa wakikebehi kilimo bila kujua bila kilimo
wasingekuwa hapo walipo. Vijana wengi wanafikiri kufanya kazi za
ofisini na wengine wanafirikiri kujiajiri katika biashara za kukaa
dukani na kusubiri wateja.
Umuhimu
wa kilimo unaonekana wazi kabisa kwani asilimia 80 ya watanzania
wanategemea kilimo, huku kilimo kikichangia asilimia 26.7 ya pato la
Taifa. Kilimo kinachangia asilimia 95 ya chakula kinachotumika
nchini, asilimia 30 ya mauzo nje na asilimia 65 ya malighafi
zinazotumika katika viwanda vyetu vya ndani Tanzania imejaaliwa kuwa
na hekta milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo lakini ni asilimia
23 tu ndio inayotumika. Kuna hekta milioni 29 zinazofaa kwa kilimo
cha umwangialiaji na maji ya kutosha yapo lakini ni asilimia 1 tu
iliyo chini ya umwangialiaji. Je, hizo sio fursa kwa kijana wanaotaka
kujiajiri kupitia kilimo?
Wapo
vijana ambao wanajishughulisha na shughuli za kilimo, vijana hawa
wamefanya shughuli hizi kwani ni mbadala baada kukosa shughuli
nyingine za kufanya. Vijana hawa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto
nyingi mojawapo ya changamoto hizi ni:-
Ukosefu wa mtaji kulima kilimo cha kibiashara.
Ukosefu wa zana bora za kilimo mfano:- Matreta.
Wadudu waaribifu wanashambulia mazao.
Kilimo cha kutegemea mvua.
Ukosefu wa taarifa mbalimbali za kilimo na fursa zilizopo.
Ulanguzi wa bei sokoni baada ya kufa kwa vyama vya ushirika.
Kutokana
na changamoto hizo ziko changamoto ambazo ziko ndani ya uwezo wa
kijana wakisasa na zipo changamoto nyingi ambazo haziko ndani ya
uwezo wa kijana.
Matatizo
haya yanaweza kutatuliwa kwa:-
Kwanza, vijana waone kuwa shughuli za kilimo ni rasmi na kijana yeyote anaweza kujiajiri kupitia shughuli za kilimo.
Vijana wafahamu fursa mbalimbali zinazotokana na kilimo.
Serikari ichukue nafasi yake kwa kutimiza nguzo kumi za KILIMO KWANZA ambazo wamezitambulisha, nguzo hizo ni:-
Utashi wa kisiasa kutoa msukumo wa mapinduzi ya kilimo
Kugharamia mapinduzi ya kilimo.
Uboreshaji wa mfumo wa utawala wa kilimo.
Mabadaliko ya mfumo wa mkakati katika kilimo.
Upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya kilimo.
Vivutio vya kuchochea uwekezaji katika kilimo.
Uendeshaji wa viwanda katika kuleta mapinduzi ya kilimo.
Sayansi, Technologia na Rasirimali watu katika kuwezesha mapinduzi ya kilimo.
Uendesha wa miundo mbinu ili kuwezesha mapinduzi ya kilimo.
Uhamasishaji na ushirikishwaji wa watanzania kuunga mkono na kutekeleza KILIMO KWANZA.
Kutokana
na umuhimu huo wa kilimo vijana wa kisasa hawapaswi kupuuza shughuli
za kilimo kwamba haziwafahi. Kilimo ni muhimu sana katika maendeleo
ya nchi yetu kwani hutupatia chakula, ajira na hukuza pato nchini kwa
ujumla.
Na.
Innocent. J. Mbele
Mwenyekiti,
FASO.
No comments:
Post a Comment