Sunday, August 12, 2012

SHIRIKA LA FASO LAFANYA SEMINA YA KILIMO KWA VIJANA KATIKA KATA YA KAHE,MOSHI VIJIJINI.

 Shirika lisilo la kiserikari la Fumbuka Agro Solution Organization (FASO) limefanya semina ya kilimo kwa vijana wa kata ya kahe moshi vijijini siku ya jumamosi, tarehe 11/08/2012. Katika semina hiyo jumla ya vijana therathini (30) kutoka vijiji 6 (kila kijiji vijana 5), vijiji hivyo ni Ngasinyi,Oria,Mawalla,Mwangaria,Kisangesangeni na Rau waliudhulia semina hiyo ya mafunzo. Akizindua semina hiyo Diwani wa kata ya Kahe Mh.Aminiel Kimati amewataka vijana kufanya kazi na kuwa wavumilivu kusubili mafanikio bila kuwa na haraka. Diwani huyo amewataka vijana waudhulie katika semina mbalimbali za maendeleo na waache tabia ya kudai posho katika semina hizo kwani semina hizo ni kwa ajili ya maendeleo yao.

Afisa kilimo na mifugo wa kata ya Kahe Bw.Lekule amewataka vijana hao kufanya kitu cha ziada baada ya semina hiyo badala ya kusikiliza na kuacha mambo hayo waliyojifunza yaishie hewani. Mkufunzi wa semina hiyo Mwl.Mushi kutoka chuo cha Kilimo na Mifugo Mwangaria aliwafundisha vijana hao jinsi ya kuchagua mazao bora kulingana na hali ya hewa ya ukanda wao. Vile vile mkufunzi huyo aliwafundisha vijana hao jinsi ya kuchagua pembejeo bora za kilimo kama mbegu, mbolea na madawa ya kuulia wadudu.

Mkurugenzi wa FASO Bw.Innocent Mbele na Meneja miradi Ndg. Moringe Allayana kwa pamoja wamewataka vijana hao kuzingatia mbinu bora za kilimo na kuacha kulima kwa mazoea. Vilevile watendaji hao wa shirika la FASO wamewataka vijana hao wajiunge katika vikundi ili wafanye kazi kwa pamoja na kunufaika na fursa mbalimbali.

Washiriki wa semina hiyo wameonyesha kufurahishwa kwa kufanyika kwa semina hiyo na wameliomba shirika la FASO kuandaa semina nyingine kama hiyo katika kata ya kahe na vitongoji vyake.


Afisa Maendeleo ya jamii kata ya kahe akimkaribisha mgeni rasmi.



Diwani wa kata ya Kahe, Mh. Aminiel Kimati (aliyesimama) akifungua semina hiyo.

 Afisa Kilimo na Mifugo Kata ya Kahe, Ndg.Lekule akiongea na wananchi.
Mwl. Mushi kutoka chuo cha Mwangaria akitoa elimu ya kilimo kwa vijana.

Mwl. Mushi akifundisha vijana.

Meneja miradi ya FASO, Ndg Moringe Allayana (kulia) na wanasemina wakifuatilia kwa makini.

Mwl.Mushi na Bw.Lekule wote kwa pamoja wakisisitiza jambo.

 Kijana wa Kahe akiuliza swali katika semina hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa FASO, Bw.Mbele akinukuhu mambo mbalimbali katika semina hiyo.

Vijana wakifuatilia kwa makini semina hiyo.


Mkurugenzi mtendaji wa FASO, Bw.Mbele (aliyechuchumaa mwisho kulia) akiwa na wana semina.

 Meneja miradi ya FASO, Bw. Moringe Allayana (aliyechuchumaa mwisho kulia) akiwa na wanasemina
Afisa Kilimo wa kata ya kahe Ndg Lekule (kushoto), Kijana wa Kahe, Mwl. Mushi na Bw.Mbele (kulia)wakiwa katika picha ya pamoja

1 comment: