Mfumo wa Kilimo cha asili aina ya Kiamba unaotumiwa na kabila la Wachaga.
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imeanzisha Mradi wa kufufua Mifumo muhimu ya asili ya kilimo Duniani (Global Importance Agricutural Heritage System- GIAHS) ili kuendeleza Kilimo cha asili (Oranic Farming) na kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji.
Mradi huo unatekelezwa na Shirika la chakula Duniani (FAO) ambao unalenga kutambua mifumo ya asili na endelevu ya kilimo na ufugaji ili kumsaidia mkulima.
Afisa Mkuu wa Kilimo kutoka Idara ya Matumizi Bora ya Ardhi Bw. Firmat Banzi
alisema mradi unagharimu zaidi ya dola laki mbili ambazo zimetolewa na Serikali ya Ujerumani.
Alisema kuwa katika Afrika Mashariki nchi ya Tanzania na Kenya ilichaguliwa kufufua mifumo hiyo kwa kuwa na sehemu muhimu za kilimo zanazotumia mifumo hiyo.
Aliongeza kuwa baada ya kuchanguliwa nchi ya Tanzani ilipendekeza mifumo mitatu ya kilimo asili ambayo ni Kihamba ambao hutumiwa na wachaga, Ndiva wa Wapare na Ngoro ambao hutumiwa na kabila la wamatengo.
Alifafanua kuwa mifumo hiyo mitatu ilifanyiwa utafiti na baadaye mfumo wa kichanga ulichaguliwa na kuanza kutumika.
Aidha, alisema kijiji cha Chimbe juu kilichopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro ndio kilichonufaika na mradi huo na sasa unafikia hatua ya mwisho katika utekelezaji wake.
Hatua hiyo imekuja baada ya tafiti mbalimbali kuonesha kushuka kwa bei ya zao la kahawa na kusema kuwa kilimo asili huongeza bei za mazao kwa kuwa mazao yanayolimwa hayatumii kemikali na badala yake hutumia mbolea ya asili kama vile samadi, aliongeza Bw. Banzi.
Mradi huo utasaidia kuboresha zao la kahawa kwa kutumia mbinu husishi za kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao.
Alifafanua kuwa mradi unajumuisha utayarishaji wa vitalu vya miche, ukarabati wa mifumo asili ya umwagiliaji na utayarishaji wa mbolea za asili kama vile samadi.
Ili kuhakikisha mradi huu unaendelea Bw. Banzi alisema wameshirikisha wadau mbalimbali ambao watasaidia kuangalia kwa karibu maendeleo ya mradi, alitaja wadau hao kuwa ni Chama cha Ushirika KNCU cha Kilimanjaro pamoja na halmashauri ya wilaya.
Mifumo ya asili ya kilimo ilianza kupendekezwa dunia toka mwaka 2002 na baadhi ya nchi zimeanza kutumia mifumo hii, baadhi ya nchi hizo ni Japani, Philipino, China na Ujerumani.
No comments:
Post a Comment