Migogoro ni hali ya kutoelewana baina ya watu Fulani katika jamii fulani. Migogoro inatokea pale watu hao wanapotofautiana mawazo ili kufikia maamuzi Fulani.migogoro hutofatiana kulingana na jamii husika,wakati,sababu/chanzo,wahusika, n.k.
SABABU ZA MIGOGORO
• Ushirikishwaji hafifu katika upangaji na utekelezaji wa shughuli za pamoja katika jamii.
• Mawasiliano duni hasa katika masuala muhimu yanoyoigusasehemu kubwa ya jamii.
• Mbinu dhaifu na zisizoendelevu juu ya utatuzi wa migogoro.
• Tabia ya kutokuwepo kwa ukweli na uwazi ambayo upelekea kutoaminiana ndani ya vikundi.
• Mahusiano ambayo hayana uwiano baina ya wadau katika shughuli za kijamii.
• Kutojiamini
• Kuwa na miundo dhaifu ya uongozi na taratibu wa kuendesha shughuli za vikundi.
• Vikundi kutokuwa na mipango ambayo haitekelezeki.
• Kuwa na katiba au miongozo yenye mianya ambayo hutumiwa vibaya na baadhi ya wanakikundi.
• Utunzaji mbovu wa kumbukumbu.
• Wanakikundi kutoheshimu na kufuata taratibu au sheria katika uendeshaji wa shughuli za vikundi.
• Baadhi ya vikundi au jumuiya kuundwa kwa shinikizo bila ya mvuto wa wanakikundi.
ATHARI ZA MIGOGORO
• Kusambaratika kwa umoja / ushirikiano katika vikundi,
• Huduma na shughuli za maendeleo kuathilika.
• Ugomvi baina ya wanavikundi,
• Migomo ambayo wakati mingine hupelekea maandamano,
WAHUSIKA WA MIGOGORO
Wahusika wa migogoro wanatofautiana kulingana na aina ya mgogoro husika.katika migogoro ya vikundi wahusika wanaweza kuwa:-
• Viongozi,
• Wanakikundi
• Serikali,mfano viongozi wa serikari za mtaa
• Wafadhili,
MIKAKATI AU NJIA ZINAZOTUMIKA KUTATUA MIGOGORO
• Kuongeza kiwango cha ushirikishwaji wa wanakikundi
• Kupelekea uamuzi kwa njia ya mazungumzo kama mbinu ya kupata suluhu endelevu
• Kujenga uwezo wa ndani wa kutatua migogoro.
• Adhabu zinazotolewa hulenga kufundisha na siyo kukomoa au kuleta chuki na mgawanyiko unaoweza kutokea kutokana na hatua hizo.
• Kutoa mafunzo kwa vikundi husika katika njia za kutatua migogoro, mafunzo pia yanaweza kutumika kama kinga ya kupunguza mifumuko ya migogoro mingine.
• Kuboresha mawasiliano katika vikundi.
• Kutoshinikiza maamuzi yoyote yale.
• Kuhakiki sifa za watu waoomba unakikundi
• Mikutano na vikao vya kikundi ifanyike kwa wakati unaokubalika kikatiba.
No comments:
Post a Comment