Friday, October 31, 2014

WAKULIMA KAHE WANUFAIKA NA MRADI WA MAHARAGE MACHANGA (FRENCH BEANS)

Shirika la FASO likishirikiana na mashirika mengine yani VECO TANZANIA na kampuni ya Frigoken yenye makao makuu yake nchini kenya, wamewawezesha wakulima wa kata ya Kahe kwa mara ya kwanza kulima maharage machanga.

Chini ya utaratibu wa kuwakopesha wakulima mbegu na vifaa vingine (k.m pembejeo) wakulima wa Kahe waliweza kuingia mkataba na kampuni ya Frigoken chini ya usimamizi wa shirika la FASO na VECO.

Wakulima hao wengi wao wakiwa vijana wameweza kunufaika kulima maharage machanga na kuiuzia kampuni ya Frigoken kulingana na mkataba waliojiwekea. ''Hii ni hatua nyingine ya maendeleo kwa mkulima mdogo kupata fursa ya kukupesheka pembejeo na kupatiwa soko, alisema Ndugu Elasto Mlayi, mkulima kiongozi wa kahe''.

 Wakulima wakikagua mazao yao
 Wakulima wakiwa kavuna maharage machanga

Wanunuzi wakiandaa vifaa tayari kununua maharage machanga kwa wakulima