Msukumo wa uhitaji mkubwa wa parachichi kwa wingi na zenye ubora unawasukuma wakulima kutumia teknolojia mpya.
Upandikizaji
hujumuisha aina mbili za mimea. Unachukua mmea mmoja ambao unadhani
hauna tija nzuri, na sehemu ya mmea mwingine ambao una ubora zaidi na
kupandikiza kwa kukata na kufunga pamoja ili kupata mbegu bora zaidi.
Utaratibu wa kupandikiza hivi sasa umekuwa silaha ya wakulima kuwakomboa
dhidi ya wadudu pamoja na magonjwa, na hili kwa sasa halifanyiki tena
maabara kama ilivyokuwa awali na hii inadhibitishwa na yale tuliyojionea
Njombe tulipotembelea wakulima.
Kwenye
shamba la bwana Bosco Kidenya, ana kitalu chenye zaidi ya miche 1200 ya
miparachichi, baadhi ikiwa tayari imeshapandikizwa na mingine ikiwa
inasubiri kufikia wakati wa kupandikiza. Huyu ni mmoja kati ya wakulima
walio wengi wanaofanya kazi kwa karibu na CARITAS Njombe, kuboresha
uzalishaji wa parachichi, pamoja na kuboresha kipato cha wakulima ambao
wanazalisha matunda na mboga mboga.
Mbinu wanayotumia
Wakulima hukusanya kokwa za parachichi
kutoka maeneo ya sokoni; wanachofanya ni kuhakikisha tu kuwa mbegu hiyo
ni safi, haijaathiriwa na magonjwa na itaota. Baada ya hapo huchagua
zile zenye muundo mzuri na kuzipanda kwenye boksi au kwenye sehemu ya
kitalu. Baada ya kuota huziotesha kwenye makopo, au kwenye viriba kisha
kuendelea kumwagilia maji mpaka zinapokuwa na umbo usawa wa penseli.
Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati mmea umefikisha unene wa penseli.
Kupandikiza kwa kutumia chipukizi lililolingana na mche unaopandikizia
ni njia yenye mafanikio zaidi.
Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati
ambao mizizi bado ni laini. Pandikizi litakalotumika wakati wa
kupandikiza ni lazima lisiwe katika hatua ya ukuaji kwa wakati huo, na
ni lazima umbo liwiane na mti linapopandikizwa kuzuia maji yasipotee na
kusababisha pandikizi kukauka.
Mapandikizi
ni lazima yatokane na aina ya parachichi ambazo zimeboreshwa kama vile
hass, fuerte au puebla. Kwa wale wakulima ambao mmea utatoa majani
mapya. wana mkataba na Africado, watahitajikupata mapandikizi kutoka
kwenye miti ya hass. Hii ina maanisha kuwa mkulima anayetaka kuanzisha
kitalu kwa ajili ya kupandikiza ni lazima apande walau miti 5 ya
parachichi aina ya hass ili kupata mapandikizi.
Njia ya kupandikiza ina ufanisi zaidi na
ni rahisi kuliko kupanda miche upya, kwa kupandikiza inagharimu chini
ya asilimia 75, kuliko kupanda miche upya na kuweza kupata aina ambayo
inastahimili magonjwa. Wakulima pia wamekuwa na rikodi nzuri ya ongezeko
la mavuno kutokana na mimea waliyopandikiza, pamoja na upungufu wa
matumizi ya madawa.
Wakulima ambao wanafanya kazi zao chini
ya CARITAS Njombe sasa wanaona faida kubwa inayotokana na kupandikiza,
wameamua kuwekeza kwenye utaalamu huu na kuwa na miche mingi kwenye
vitalu vyao. Hii ni mbinu ya kilimo ambayo ina faida kubwa kwa mkulima,
huku akiwa amewekeza kwa kiasi kidogo sana katika kukabiliana na wadudu
na magonjwa na kuepuka kuwa na mazao yenye ubora wa chini.
• Nafasi halisi inayohitajika na mmea wa parachichi ili ukae vizuri ni nafasi ya 9m x 9m. Chimba shimo katika vipimo vya 60sm x 60sm kwa 60sm kwenda chini kisha tenga udongo wa juu na wa chini. Changanya udongo wa juu na mbolea ndoo moja iliyooza vizuri, pamoja na kiganja kilichojaa cha mbolea ya minjingu.
• Ondoa mche wako kwenye kiriba ulipopandwa. Hii itakuwa rahisi zaidi endapo ulikuwa umenyweshea muda kidogo uliopita. Panda kwa kutumia udongo wa juu uliochanganya na mbolea na uweke mpaka kujaza shimo.
No comments:
Post a Comment