Mkulima atapata faida kubwa ikiwa atatunza zao la nyanya kwa uangalifu mkubwa.
Nyanya
huzaa vizuri sana hasa zinapowekewa mbolea mboji au samadi iliyooza
vizuri. Unaweza kuongeza mbolea ya minjingu kiasi cha kijiko kimoja cha
chakula au vijiko 3 vya chai kwa kila shimo. Endapo ardhi ina upungufu
wa mbolea asili, inashauriwa kupanda kwanza mimea yenye uwezo wa kutoa
mbolea vunde bora kama vile kunde, mucuna, soya au clotalaria kabla ya
kusia mbegu za nyanya au kupanda. Epuka mbolea za viwandani kwa kuwa
nitrojeni ikizidi husababisha nyanya kuvimba, na baadaye kuoza kirahisi,
pia husababisha mnyanya kukua kupita kawaida. Kuwa na nitrojeni
iliyozidi kwenye udongo pia husababisha majani kuwa laini sana hivyo
kuvutia wadudu na magonjwa kirahisi. Ushindani wa magugu dhidi ya nyanya
zako unakuwa ni mkubwa sana, hasa sehemu zenye joto na unyevu mwingi.
Ili kudhibiti magugu kwenye eneo
lililo wazi, fyeka mara kwa mara na uhakikishe kuwa ni mafupi kuliko
nyanya mpaka hapo nyanya zitakapokomaa na kuiva. Acha magugu uliyofyeka
kwenye shamba lako yawe kama matandazo ili kusaidia kupunguza au kuzuia
mmomonyoko wa ardhi, kupunguza joto kwenye ardhi na kuhifadhi unyevu
kwenye udongo. Hii inaweza pia kufanywa kwa kupalilia kwa mikono
katikati ya mistari ya nyanya, na kuweka matandazo hayo katikati ya
mistari.
Fito
Kwa aina ya nyanya zinazorefuka sana,
chomeka walau fito zenye urefu wa mita 2 katika kila mche wa nyanya na
ufungie kwa kutumia kamba. Badala yake unaweza kutengeneza kichanja
chenye nyaya na nguzo kila baada ya mita 1 au 2 na nyingine yenye urefu
wa mita 0.15 kutoka ardhini. Funga kamba imara kwa kila mnyanya. Mnyanya
unaweza kuzungushwa kwa uangalifu mkubwa kwenye kamba hiyo kulingana na
unavyokuwa.
Kukatia matawi ni muhimu sana kwa
aina zote za nyanya. Unaweza kuacha shina kukua na kukata matawi mawili
ya awali ili kuruhusu mmea kukua vizuri. Kata matawi kulingana na mmea
unavyokuwa kwa wiki. Mmea unapokuwa na viriba 6 au 8 vya maua ni vizuri
kukata kichwa ili kuwezesha ukuaji mzuri matunda yatakayotokea ambayo
yatakuwa na soko zuri. Majani yaliyo karibu na ardhi ni lazima
yaondolewe ili kusaidia kuzuia uwezekano wa mabaka kuingia kwenye mmea
na matunda. Hakuna kanuni za kukata matawi au kupata idadi flani ya
matunda kwa kila mmea, hii inategemeana na mkulima na aina ya nyanya.
Nyanya zinahitaji umwagiliaji mzuri katika siku za mwanzo toka kupandwa,
wakati wa kuchanua, na wakati wa kukuza matunda. Kupatikana kwa maji ya
kutosha kwenye minyanya, husaidia kwa kiasi kikubwa kuwa na mazao na
kukomaa kwa wakati mmoja. Husaidia pia kupunguza uwezekano wa kuvimba
na kuoza kwa nyanya, muonekano usiokuwa wa kawaida hutokana na ukosefu
wa kalishamu ya kutosha wakati wa kutengeneza na kukuza matunda. Wakati
wa kiangazi, ni muhimu kunyweshea angalau mara mbili kwa wiki. Unyeshaji
kwa njia ya matone ni njia bora zaidi na isiyokuwa na madhara
ukilinganisha na umwagiliaji wa mifereji, hii ni kwa sababu maji
hudondoka kidogo kidogo kwenye shina.
Kuvuna
Nyanya kwa ajili ya kuuza zinaweza
kuvunwa zikiwa bado na rangi ya kijani baada ya kukomaa, kisha zinaweza
kuiva zikiwa zinasafirishwa kwenda sokoni, au zikahifadhiwa kwanza ili
ziive. Nyanya zinazotumika kwa ajili ya kutengeneza supu, juisi, na
mchuzi huachwa shambani mpaka ziive kiasi cha asilimia 85. Nyanya
huchumwa zikiwa bado ngumu, lakini kiasi cha asilimia 65 huwa tayari
kuchumwa kwa wakati mmoja.
Wadudu wa nyanya na njia za asili za kudhibiti
Hawa ni wadudu hatari wanaoshambulia vitalu vya nyanya. Wanakata shina la mimea iliyooteshwa au inayoota.
Ni nini cha kufanya;
• Ondoa magugu mapema, angalau wiki mbili kabla ya kupanda.
• Chimbua na utifue vizuri shamba lako kabla ya kupanda. Hii inasaidia kuwaibua sota na kufanya waliwe na maadui zao.
• Tengeneza wigo kulinda miche
iliyohamishwa na kupandwa shambani. Wigo unaweza kutengenezwa kwa
kuzungushia karatasi, karatasi ya foili, au ubao mwepesi kuzunguka
sehemu ya bustani.
• Chimba karibu ya mimea iliyoharibiwa na uwateketeze sota.
• Wahifadhi wadudu wa asili wanaokula sota.
Vidukari hunyonya maji kwenye mimea na kusababisha mimea kupunguza uwezo wa kukua, pia hutoa ute kama asali, ambao husababisha unga unga unaosababisha mimea kukakamaa. Unga huu kwenye matunda husababisha yasipate soko.
Ni nini cha kufanya;
• Tunza wadudu wa asili wanaokula
vidukari. Epuka kutumia madawa kwa wingi kwani yanaweza kuua wadudu wa
asili wanaodhibiti vidukari.
• Tumia matandazo yanayong’aa. Vitu vinavyo akisi mwanga kama vile aluminiamu, husaidia vidukari wasiwezi kutua kwenye mimea.
Root knot huathiri sana
nyanya. Madhara yanakuwa makubwa zaidi sehemu yenye udongo wa kichanga
na kunyeshea kwa kutuamisha maji. Minyoo husababisha vifundo kwenye
mizizi. Mimea iliyoathiriwa hunyauka, na wakati mwingine hufa kabisa
wakati wa jua.
Ni nini cha kufanya;
• Fanya mzunguko wa nyanya na nafaka.
• Usiweke kitalu cha miche mahali ambapo unahisi kuwepo magonjwa.
• Tumia aina ya nyanya inayostahimili magonjwa.
• Panda mazao mseto.
• Hakikisha kuna kiasi cha kutosha cha mbolea asili kwenye udongo.
Chanzo: Mkulima Mbunifu
No comments:
Post a Comment