Pages

Friday, February 17, 2012

Maghembe: Mchango wa kilimo kwenye Pato la Taifa hauridhishi

WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe amesema kuwa kiwango ambacho sekta ya kilimo inachangia katika Pato la Taifa hakiridhishi, hali inayoonyesha biashara si nzuri katika eneo hilo. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Prof Maghembe alisema kuwa kazi kubwa inahitajika kufanyika katika sekta hiyo ili kuweza kuongeza uchangiaji wake katika Pato la Taifa. Alisema asilimia nne ambayo sekta hiyo inachangia katika Pato la Taifa wakati asilimia 85 ya Watanzania wanategemea kilimo kupata kipato chao, ni wazi bado nchi iko nyuma katika eneo hilo. "Asilimia hiyo nne inaonekana ni kitu kikubwa na sekta inakuwa vizuri. Lakini bado kwa nafasi hiyo kiasi tunachozalisha ni kidogo na hakitoshi," alisema Prof Maghembe na kuongeza; "Nia yetu kwenye kilimo siyo urembo wala mitindo bali ni biashara ambayo inahitaji kubadilika na ndiyo maana tumekiweka kuwa namba moja." Maghembe alisema kumekuwa na matatizo ya kutokuwepo chakula cha kutosha lakini Serikali imejitahidi kuhakikisha wananchi hawafi kwa njaa na imeweza kutoa chakula kwa asilimia 95 kwa wanan Chanzo: Mwananchi

No comments:

Post a Comment