Pages

Friday, September 24, 2010

VIJANA WA TANZANIA BILA UMASIKINI INAWEZEKANA?

UMASIKINI NI NINI?
Watu tofauti hufasiri maana ya umasikini kwa njia mbalimbali viongozi kwa kawaida hufikiria juu ya umasikini kwa kuangalia uwezo wa watu katika kununua mahitaji yao na kuuza bidhaa zao. Lakini fasiri ya umasikini ni kubwa zaidi. Kuna fasiri ya kuzingatia matatizo ya kuwa na mgawanyo sawa katika kupata elimu na afya bora, kuwa na heshima na hadhi katika jamii, kusikia kuwa na uwezo na kutatua tatizo lolote linalotokea katika maisha yake, na hivyo kuwa na matumaini ya maisha. Kwa hiyo kuna mengi ya kufikiria wakati unapotaka kuondoa umasikini. Kwa hakika fikra nyingi haziko wazi mpaka unapofikiria kwa makini yanayotendeka katika jamii.

Watu wa kawaida, wafanyabiashara, wafanyakazi serikarini, mawaziri na viongozi wa nje wana mawazo tofauti kuhusu swali la umasikini ni nini. Wana mawazo tofauti kuhusu sababu za umasikini na jinsi ya kuondoa.

Wataalamu wanavyolioa suala la Umasikini
Katika dunia ya sasa watu hununua mahitaji yao kwa kutumia pesa. Kama hawana njia za kupata pesa watakuwa maskini. Umasikini mbaya zaidi ni ule ambao unawafanya watu wasiweze kupata chakula. Kwa hali hiyo, wanakuwa dhaifu na wanaweza kufa kwa njaa. Hali nyingine ya umasikini ni ile ambayo watu wanaweza kuwa na chakula kiasi au kidogo lakini hawana maji salama, huduma za matibabu, nyumba au mavazi bora.

AINA YA UMASIKINI
Umasikini wa kipato
Inafikiriwa kuwa wakati mapato ya watu ni chini ya dola moja kwa siku katika nchi zinazoendelea kama Tanzania. Hii ina maana kwamba hawatakuwa na chakula cha kutosha, uwezo wa kupata tiba, watakuwa na mavazi na nyumba duni.

Umasikini usioo wa kipato
Kuna wakati watu wanakuwa na fedha kidogo na hivyo hawawezi kumudu shule nzuri na kuwa na maji salama watu wanaoishi katika umasikini usio na kipato wanategemewa kudumaa na kufa mapema.


Tutapunguzaje umasikini?
Vijana wengi walipoulizwa wajiepushe na nini ili wasiingie katika hali ya umasikini walitoa mawazo yafuatayo:-
Wamiliki ardhi.
Wapate zana za kilimo na technologia..
Waweza kupata masoko kwa urahisi.
Wapate misaada na mikopo.
Kujenga uwezo wa kuweka akiba.
Waweze kupata maji safi na salama.
Wawe na usafiri nzuri (barabara na magari).
Kupunguza rushwa, kuwe na uwazi zaidi, kuimarisha uwajibikaji na ushirikishwaji katika kuchangia kutoa maamuzi katika kiwango cha serikari za mitaa na serikari kuu.
Wapate huduma bora za jamii na miundo misingi (hasa afya na elimu).
Kuunda upya na kuimarisha vyama vya ushirika.
Kuwawezesha wanawake wawe na madaraka zaidi katika kudhibiti mali ya familia.
Kujenga umoja, mshikamano, kuaminiana na hali ya kushirikiana.
Usalama kazini.

Hata hivyo umasikini unaweza kuondilewa kwa kutatua matatizo yafuatayo:-
Kushughulikia tatizo la ajira kwa vijana.
Kuzuia uharibifu wa mazingira.
Serikari kuongeza fedha zilizopo (bajeti) kwa ajili ya kuondoa umasikini.
Kuendeleza mfuko wa fedha ili kusaidia wakulima wadogo wadogo.
Kuwasaidia watu kuendeleza biashara ya kati.
Kuifanya utafiti zaidi ili kugundua jambo gani linapaswa. Kufanywa na tuna uwezo gani wa kulifanya jambo hilo.
Kuzuia ajira kwa watoto.
Kuongeza idadi ya wanafunzi wanajiunga shule za sekondari na vyuo mbalimbali.

Nafasi ya kijana mmoja mmoja katika kupunguza umasikini
Licha ya serikari kuwajibika katika kupunguza umasikini kwa wananchi wake, ipo nafasi ya kijana mmoja mmoja katika kupunguza umasikini:-
Kutafuta uwezo wa kujiajiri.
Kuwa wabunifu katika kazi zao
Kutafuta taarifa na fursa mbalimbali.mf. Soko la Afrika mashariki
Kuungana katika vikundi ili kufanya kazi pamoja.
Kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kushiriki katika kufanya uwamuzi wa mambo yanayowahusu.
Kupanga na kutumia muda vizuri.

Kama hayo yote yatafanyika, serikari, wahisani na vijana wenyewe kushiriki katika kutatua swala la umasikini, jibu litakuwa VIJANA WA TANZANIA BILA UMASKINI INAWEZEKANA.

No comments:

Post a Comment