Uelewa wa maisha ya mimea husaidia kwa kiasi kikubwa kwa hatua ya kuchukua kuilisha mimea hiyo.
Utunzaji
wa udongo unategemeana kwa kiasi kikubwa na mazingira ya kibiolojia.
Kazi kubwa ya baadhi ya viumbe hai waliomo kwenye udongo, ni kumeng’enya
mabaki ya mimea na viumbe hai wengine. Mtiririko huu hufanya uwepo wa
nguvu, virutubisho, na hewa ya kaboni, ambavyo kwa pamoja hutengeneza
rutuba kwenye udongo.
Utunzaji wa rutuba ya udongo
unaongozwa na filosofia hii ‘Lisha udongo ili nao ulishe mimea.’ Udongo
wenye rutuba utazalisha mimea yenye afya inayoweza kukabiliana na
magonjwa. Uzalishaji wa mazao kwa njia za asili uhakikisha kunakuwepo
uzalishaji wa kutosha bila ya kutumia pembejeo za ziada isipokuwa
matandazo, mboji na bila kutifua udongo mara kwa mara. Ongezeko la
malighafi za asili husaidia kuimarisha udongo na kufanya kuwepo kwa
virutubisho vya kutosha.
Athari kwa afya ya mimea
Kwa bahati mbaya, aina ya kilimo cha
kisasa na kinachotumia kemikali hufanywa tofauti na ilivyo kwa kilimo
hai. Katika aina hii ya kilimo; udongo hulimwa mara kwa mara jambo
linalosababisha uharibifu wa muundo wa udongo, uwiano wa virutubisho,
ambapo virutubisho huongezwa kwa kutumia mbolea za viwandani na
matandazo hayazingatiwi. Muundo wa udongo unapobadilika, rutuba nayo
hupungua, uwezo wa udongo kwenye udongo pia hupungua.
Kiwango cha udongo mzuri pia
hupungua kwa kuwa hakuna tena viumbe hai wanaotengeneza udongo ila
unapungua kila msimu wa mavuno. Kwa asili mzunguko huu huwa na matokeo
yanayoishia kwenye afya ya mimea, na hapa wadudu huchukua nafasi
inayowawezesha kufikia malengo yao.
Ziba pengo
Wakulima wanatakiwa kuhakikisha kuwa
kuna virutubisho vya kutosha shambani mwao kila wakati. Ikiwa kuna
mwanya pale ambapo baadhi ya pembejeo zinakosekana, kununua virutubisho
kwa ajili ya udongo vilivyomo kwenye mfumo wa mbolea za asili
inaruhusiwa. Hata hivyo, weka utaratibu wa kuwa na virutubisho kutoka
shambani mwako muda wote.
Endapo tukitegemea kulisha udongo
kutokana na mbolea za viwandani na kutumia virutubisho vya asili, bado
tutakuwa tunafanya sawa na yanayofanyika katika kilimo cha kisasa.
Tutakuwa hatujauongezea udongo uwezo wa kujitengeneza na kuongezeka,
jambo ambalo ndio msingi muhimu wa kilimo hai.
Vyanzo vya virutubisho
Mimea inayofunika udongo – Mimea inayotambaa huongeza na kushika virutubisho kwenye udongo, kuongeza malighafi zinazooza kwenye udongo, kuzuia madini ya naitraiti kuzama kwenye udongo, virutubisho kutiririshwa, na mmomonyoko wa udongo. Jambo la muhimu hapa ni kuwa udongo umefunikwa ili kuzuia uharibifu. Mimea jamii ya mikunde inapendekezwa zaidi kwa kuwa
husaidia kuongeza nitrojeni kwenye udongo inayopatikana hewani.
Inashauriwa pia kuchanganya mimea jamii
ya mikunde na nyasi kwa kuwa nyasi hutumia nitrojeni nyingi sana kutoka
kwenye udongo, hivyo itasaidia kutokuharibika kwa mtiririko mzima wa
uwekaji wa nitrojeni kwenye udongo.
Mboji -
Mboji hasa inayotengenezwa kwa kutumia kinyesi cha wanyama, inaweza
kuwa chanzo kizuri cha viumbe wadogo kwenye udongo na virutubisho vyenye
gharama ndogo. Unapotumia mboji, changamoto kubwa ni kuhakikisha kuwa
imeoza vizuri na namna ya kuitumia kwa usahihi. Endapo mchanganyiko
uliotumika kutengeneza mboji hiyo yalikuwa na ubora wa chini, basi mboji
hiyo nayo itakuwa na ubora mdogo sana. Itakuwa vizuri kama wakulima
hawataacha mboji ikapigwa na jua au mvua, kwa kuwa hali hii inaweza
kusababisha kupotea kwa virutubisho kwenye mboji. Kinyesi cha mifugo
huboresha mboji zaidi.
Utafiti wa hivi karibuni unaonesha
kuwa kiasi cha 15% ya virutubisho vinavyopatikana kwenye mboji hutumika
shambani kwa mwaka wa kwanza. Hivyo, matumizi ya mara kwa mara ya mboji
yanapendekezwa ili kuweza kuongeza nitrojeni na malighafi zinazo oza
kwenye udongo.
Samadi -
Samadi inayotokana na wanyama waliokomaa inaweza kuwa na uwiano mzuri wa
virutubisho vya nitrojeni na aina nyingine kwa kiasi kidogo. Tatizo
moja la samadi ni upatikanaji pamoja na kutokuwa na ubora unaofanana
wakati wote. Kiasi kikubwa cha samadi inayotumika kwenye shamba la
mboga, huozeshwa kabla ya kutumika, jambo linalosaidia kupunguza madhara
kwenye vyakula.
Malengo kwa ajili ya udongo na mazao
• Kuongeza malighafi zinazo oza kwenye udongo
• Kuboresha muundo wa udongo
• Kuwezesha upatikanaji wa nitrojeni
• Kuongeza uwezo wa uhifadhi wa rutuba
• Kujenga uwepo wa uhai wa viumbe hai kwenye udongo
• Kufifisha magonjwa ya mazao
• Kujenga mazingira ya udongo wenye uwiano
Chanzo: Mkulima Mbunifu
No comments:
Post a Comment