Pages

Monday, July 9, 2012

FASO YAFANYA ZIARA KUTEMBELEA WAKULIMA.


SHIRIKA LA FASO LIMEFANYA ZIARA KUTEMBELEA KIKUNDI CHA WAKULIMA "MSHIKAMANO GROUP" KINACHOFANYA SHUGHULI ZAKE MAENEO YA MSARANGA, MOSHI. KIKUNDI HICHO KINAJIHUSISHA NA KILIMO CHA MBOGAMBOGA NA KINAJUMUISHA WANACHAMA MBALIMBALI WENGIWAO WAKIWA VIJANA. LENGO LA ZIARA HIYO NI KUJENGA UKARIBU WA KIUTENDAJI KATI YA SHIRIKA NA WAKULIMA. VILE VILE KUTOA USHAURI NA KUJUA MATATIZO YANAYOWAKABILI WAKULIMA HAO WADOGO.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la FASO akikaguwa mifereji ya maji inayotumiwa na wakulima wa kikundi cha MSHIKAMANO















Meneja miradi ya FASO Bw.Moringe Allayana akiwa na wakulima wa MSHIKAMANO GROUP

FASO YATOA SEMINA KWA WAKAZI WA RAU.

Katika kuendeleza harakati za kuleta mabadiliko (hasa kiuchumi)  katika jamii FASO ilitoa semina fupi kwa wakazi wa kata ya RAU MADUKANI, Moshi mjini. Semina hiyo ilihusu kushawishi wananchi kujiunga katika vikundi vya kuweka na kukopoa (VICOBA). Semina ilifanyika katika mkutano wa hadhara wa kata ya RAU ulioitishwa na viongozi wa kata hiyo viwanja vya RAU madukani mjini Moshi..


 MKURUGENZI MTENDAJI WA FASO NDG. INNOCENT MBELE AKITOA SEMINA HIYO KWA WAKAZI WA RAU.
WAKAZI WA RAU KATIKA SEMINA YA VICOBA.